Kukutazama, Ukitabasamu Nikama kuwatch movie za afro, siwezi boeka We ndo kitabu, Mi ndo kalamu Niliumbwa kwa ajili yako, Kama masai na Rubeka Ninatamani ningewa yako mavazi Nikusitiri nikuguse Kila wakati Ungewa stew ama kasupu ka mbaazi Ningewa sembe Mokimo ama chapati
Baki na Mimi kipenzi, nikushughulikie Kila asubihi, nirauke, ili nikupikie Nikuogeshe, nikuvishe, mpaka uvutie Kamba za viatu babe, mi nikufungie
(Baki namimi) ntangangana nikuwe chochote unachotamani (Ooh Baki namimi) nitakonda utavimba, utakopa ntalipa mama (Baki na Mimi) naapa kukutunza kuliko wako wa zamani (Ooh Baki na Mimi) ukisota ntaiba, Utapona nna tiba mamaa
Nakama ungewa, mwanasiasa, ninge piga kampeni zako Nikusifie, kwa giza na mwangaza, mpaka kwa maadui zako Nitakubusu bila woga hadharani Ili wajue wewe ndo wangu mwandani Ungewa kijiko lazma ningewa sahani Kututenganisha Hilo haliwezekani
Baki na Mimi kipenzi, nikushughulikie Kila asubihi, nirauke, ili nikupikie Nikuogeshe, nikuvishe, mpaka uvutie Na ukichoka, nikubebe, wivu wasikie